Beki wa Brazil na klabu ya PSG, David Luiz uwenda akarejea Chelsea msimu huu baada ya klabu hiyo kuonesha nia ya kutaka kumsajili ambapo wameweka paundi milioni 30 kumrudisha Darajani beki huyo.

Beki huyo aliihama Chelsea na kuelekea Ufaransa miaka miwili iliyopita baada ya kusajiliwa na PSG kwa ada ya uamisho ya paundi milioni 50 na kuwa beki ghali duniani kwa kununuliwa kwa bei kubwa.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anataka kumsajili beki huyo wa kati abaada ya dili la kumsajili beki wa AC Milani, Alessio Romagnoli na Kalidou Koulibaly kutoka Napoli kushindikana.

David Luiz alisajiliwa na Chelsea mwaka 2011 kutoka klabu ya Benfica kwa ada ya uamisho ya paundi milioni 21, alidumu kwenye klabu hiyo kwa miaka mitatu kabla ajatimkia PSG ya Ufaransa ambapo alicheza mechi 143 na kushinda magoli 12.

Davidi Luiz ameisaidia timu yake PSG kushinda ligi kuu Ufaransa maarufu kama ligi 1 msimu uliopita pamoja na kufika robo fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Beki huyo aliondoka klabu ya Chelsea kwasababu alikuwa hayupo kwenye mipango ya aliyekuwa kocha wa wakati huo Jose Mourinho ambaye kwasasa anaifundisha klabu ya Manchester United.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *