Klabu ya Chelsea imemsajili kwa mara ya pili beki wa kimataifa wa Brazil, David Luiz kutoka Paris St-Germain kwa ada ya uhamisho paundi milioni 30 kwa mkataba wa miaka mitatu.

David Luiz amefuzu vipimo vya afya kwenye klabu hiyo dakika tano kabla ya dirisha la usajili alijafungwa barani Ulaya.

Baada ya usajili huo kukamilika beki huyo amesema kwamba anashukuru kurejea tena katika klabu yake ya zamani huku akiongeza kuwa ana imani na kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte.

Beki huyo aliuzwa kuelekea klabu ya PSG miaka miwili iliyopita kwa ada ya uamisho ya paundi milioni 50 na kuweka rekodi ya kuwa beki wa kwanza kununuliwa kwa bei kubwa duniani.

Wakati alipokuwa Chelsea kabla ajaelekea PSG, David Luiz alicheza mechi 143 na kushinda magoli 12 na klabu hiyo ya darajani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *