Mkali wa ngoma ya ‘Muziki’ Darassa amesema kuwa hakutoa ngoma mpya kwa lengo la kufunika ngoma ya mtu mwingine bali ni kufikisha ujumbe kwa jamii na kuwaburudisha mashabiki wake.

Darassa amefunguka hilo katika kipindi cha FNL cha EATV alipotakiwa kufafanua iwapo ni kweli kwamba alitoa ngoma hiyo ili kufunika ngoma ya msanii mingine mkubwa wa bongo fleva iliyotoka kipindi hichohicho.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakizilinganisha baadhi nyimbo mpya zilizotoka hivi karibuni ambapo wimbo wa Darassa umekuwa ukilinganishwa na ngoma ya Kokoro iliyotolewa na Rich Mavoko akimshirikisha Diamond.

Mashabiki wengi wamekuwa wakidai kuwa ngoma ya Muziki ya Darassa imeifunika ngoma hiyo ya Kokoro.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *