Mkali wa hip hop Bongo, Darassa leo amefanya show ya bure katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na mashabiki wake maeneo hayo.

Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa alitoa burudani ya kufa mtu baada ya kuimba vipande vya nyimbo yake ‘Muziki’ inayofanya vizuri.

Darassa: Mashabiki waliojitokeza kwenye shoo ya bure ya Darassa.
Darassa: Mashabiki waliojitokeza kwenye shoo ya bure ya Darassa.

Darassa na Roma wanatarajiwa kutoa burudani katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam siku mkesha wa mwaka mpya.

Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada,  Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *