Mwanamuziki wa Bongo fleva, Darassa amesema kuwa anatarajia kufanya mazuri mwaka 2017 kama alivyofanya mwaka jana kwenye game ya Bongo fleva baada ya kupata mafanikio kwa muda mfupi.

Kupitia akanti yake ya Instagram Darassa ameelezea hisia zake kwenye game ya Bongo fleva endapo atajaliwa afya katika mwaka huu mpya.

Katika ukurasa wake wa Instagram Darassa ameandika ujumbe ambao unasomeka “2017 miujiza inaendelea”┬áhuku baadhi ya mashabiki wake wakitafsiri kuwa rapa huyo ataendelea kufanya vyema na kufanya kazi ambazo huenda zikawashangaza tena kama ilivyokuwa kwa ngoma yake ya ‘Muziki’.

Mwaka 2016 ni mwaka wa historia kwa Darassa rapa ambaye amejipatia umaarufu zaidi na kufanya show nyingi huku akishuhudia mambo makubwa zaidi katika muziki wake toka alipoanza kufanya muziki.

Darassa mwenyewe anakiri wazi kuwa mwaka 2016 kwake ulikuwa mwaka wa miujiza kwa jinsi ambavyo ameweza kuja na kubadili upepo wa muziki wa Tanzania na kuingia katika akili za watanzania walio wengi kutokana na kazi yake ya ‘Muziki’ ambayo imefanya mengi makubwa ndani ya muda mfupi sana.

.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *