Jumla ya wanafunzi 917,072 wanatarajia kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi hapo kesho ambapo utafanyika Septemba   6 na 7  nchi nzima.

Katibu Mtendaji wa baraza la mitihani Dr Charles Msonde amesema maandalizi kwaajili ya mitihani huo umekamilika ikiwa ni pamoja na kusambaza karatasi za mitihani, fomu maalumu za kujibia mitihani na nyaraka zote muhimu kwaajili ya mtihani huo.

Msonde ametoa onyo kali kwa wasimamizi wa mitihani, waalimu, wananchi na wamiliki wa shule watakao jaribu kufanya udanganyifu kuwa watachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kufungia shule zote zitakazofanya udanganyifu.

Masomo yatakayo tahiniwa ni Kiswahili, English Language, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *