Staa wa Hip Hop nchini, Darasa amesema kuwa kwa sasa anafanya vizuri kwenye game ya muziki kutokana na changamoto alizopitia kwenye maisha yake ambazo zimempelekea kufanya kazi kwa kujituma.

 

Darasa amesema moja ya vitu ambavyo vilimpa changamoto ya kupambana ni pamoja na kukosa chakula, sehemu ya kulala hata kukosa malazi wakati huo kabla ajaanza muziki.

 

Staa huyo amesema changamoto hizo zimezidi kumpa hasira mpaka sasa ya kuendelea kufanya vyema katika kazi yake ya muziki.

 

Darasa amesema changamoto zina njia mbili zinaweza kukuua kabisa au zikakufanya kuwa bora zaidi lakini siku zote mtu mwenye malengo changamoto haziwezi kumuua bali zinamfanya kuwa bora zaidi.

 

darasa

Vile vile amesisitiza kwa kusema kazi yoyote nzuri ambayo saizi inafanya vizuri ni kutokana na changamoto ambazo amepitia nyuma kama kulala njaa nyumbani ama kukosa sehemu ya kulala.

 

Mbali na hilo Darasa amewataka vijana kuwa na malengo ya maisha na kutokatishwa tamaa na changamoto ambazo wanakutana nazo bali wanapaswa kupambana nazo ili kufikia malengo yao.

 

Msanii huyo kwa sasa anatamba na wimbo wake ‘Too much’ unaofanya vizuri katika vituo mbali mbali vya Radio na Runinga nchini.

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *