Mwanamuziki wa hip hop nchini, Darasa ameguswa na taarifa za vijana waliokamatwa mkoani Singida waliokuwa wakiendesha gari huku wakicheza nyimbo yake mpya inayofanya vizuri kwasasa ‘Muziki’.

Taarifa iliyopo ni kwamba vijana hao wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida likiwashikilia kwa mahojiano ili sheria ichukue mkondo wake kutokana na kosa hilo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Darassa ameoneshwa kuguswa na tukio la kukamatwa kwa vijana hao mkoani Singida.

Darasa ameandika “Hawa ndugu zetu nimepata taarifa wamekamatwa kwa kosa la kutaka kusababisha ajali na unaweza kuona Kama mchezo ulielekea kubaya, ingeweza kua Tatizo kwao Au kumu sababishia mwingine, Naskia watakua mahakamani Leo I’m not so sure naendelea kufatilia”

Pia ameongeza “Nawaombea Tatizo hili Mungu awafanyie wepesi I’m sure wamejifunza Hawawezi kufanya tena mistake Kama Hii itokee, mizuka feelings mtu anaweza kufanya kitu njee ya mipango yake sometimes, Mungu awasaidie  LENGO NI KUJENGA DUNIA KUA SEHEMU NZURI NA SALAMA KUISHI #Muziki“

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *