Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Mrisho Gambo amechukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa hapo jana.

Ntibenda kwasasa anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambapo sherehe za kuapishwa kwake zimefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *