Bendi ya Dar Music inatarajia kufanya uzinduzi wake katika ukumbi wa Mango Gardeni jijini Dar es Salaam Septemba 16 mwaka huu ambapo watasindikizwa na staa wa Taarab Khadija Kopa pamoja na bendi kongwe ya Msondo.

Uzinduzi huo utaenda sambamba na utambulisho wa albamu ya bendi hiyo iliyobeba nyimbo 6 pamoja na video ya wimbo wao wa Chozi la Maskini.

Meneja wa bendi hiyo Khamis Maero amesema kuwa uzinduzi huo mkubwa unafanyika kwa mara ya kwanza toka rais mpya Jado Fideforce aingie madarakani.

Amesema kuwa utambulisho huo pia utatumika kwa ajili ya kutambulisha wanamuziki wapya waliojinga na bendi hiyo.

Kiongozi wa bendi hiyo Edward Anthony ‘Fide Force’ alisema kuwa nyimbo zitakazotmbulishwa katika uzinduzi huo ni pamoja na wimbo uliobeba albamu yao ya Chozi la Maskini pamoja na Salmaga.

Nyimbo nyingine ni Bongo mchango, Maisha Upendo, Mtu Box, Jibebishe  na Ama zao Ama zangu.
Amesema ndani ya bendi yake ameamua kuchukua wanamuziki wazuri ili kuifanya kuwa bora zaidi.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa ana uzoefu mkubwa na kile kinachopelekea bendi nyingi kuvunjika hivyo hawawezi kuruhusu kitu hicho kitokee ndani ya bendi yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *