Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kupokea timu ya taifa ya kuogelea ambapo inarudi kesho ikitokea Rio de Janeiro Brazil ilipokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki.

Timu hiyo inayoundwa na wachezaji wawili Hilal Hilal na Magdalena Moshi ilitarajiwa kuondoka jana kutoka katika jiji hilo kuelekea Sao Paulo kisha leo kuwasili Dubai na kesho itawasili Dar es Salaam kuanzia saa tisa alasiri.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka, timu hiyo ikiwasili italakiwa na Watanzania wakiongozwa na Makonda ili kuwatia moyo kwa kile ambacho wamefanya kwenye michezo hiyo.

Katibu mkuu huyo amesema anaomba watu wajitokeze uwanja wa ndege ili kuwapa mapokezi makubwa wachezaji hao.

Hilal alifanya vizuri katika kundi lake na kuweka rekodi mpya ya taifa kwa sekunde 23.70 katika mtindo wa Freestyle mita 50 ambayo haikuwahi kuwekwa na Mtanzania yeyote, hata hivyo hakufanikiwa kuvunja rekodi ya muda wa kimataifa.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *