Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi ramani ya jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ikiwa ni ahadi ya kuwajengea jengo hilo.

Makonda amesema jengo hilo linatarajiwa kuwa na ghorofa tatu na litagharimu zaidi ya Sh bilioni tano na Ijumaa ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi huo huku akisema ujenzi huo utaanza hivi karibuni kukamilika kwa muda usiozidi miezi 14.

Makonda pia amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuhubiri amani ili taifa liendelee kuwa na amani na mshikamano.

Mkuu wa mkoa huyo amesema ujenzi wa jengo hilo, umekuja baada ya kuona kuwa Bakwata imekuwa na mchango mkubwa kwa taifa ikiwemo kuhubiri amani na mshikamano.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *