Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro amewataka wananchi kuondoa hofu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani hakuna atakayeandamana Septemba 1.

Kamanda Siro amesema Jeshi hilo lipo imara kuhakikisha hakuna mtu atakayethubutu kuingia barabarani kuandamana.

Siro amesema kuwa habari ya UKUTA haipo umeshabomoka na kama aujabomoka utabomoka tu kwa hiyo wakazi wa Dar es Salaam wasiwe na hofu wafanye kazi zao kama kawaida kwani hakuna atakayejitokeza barabarani kuandanama.

Pia kamanda Siro ameeleza kuwa Jeshi hilo limekamata fulana zenye ujumbe zinazochochea maandamano hayo zilizoandikwa “TUJIPANGE TUKATAE UDIKTETA UCHWARA”  ‘UKUTA’.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wametangza siku ya Septemba 1 ni siku ya maandamano na mikutano nchi nzima kwa kile walichodai kunyimwa uhuru wa kidemokrasia ndani na nje ya Bunge.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *