Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee amepongeza hatua ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kwa kuonesha nia ya kutafuta suluhisho baina ya wabunge wa upinzani na serikali.

 

Mbunge huyo amesema nia hiyo ni njema lakini azma hiyo lazima izingatie mahitaji ya pande zote mbili ili kupata muafaka.

 

Mdee amesema anaamini utekelezaji wake hautakuwa wa kibaguzi na upendeleo bali utaangalia zaidi pande zote mbili kwa lengo la uendeshaji bora wa shughuli za Bunge.

 

Pia amesema kuwe na dhamira ya kweli kutoka kwa Spika ili kiongozi huyo akirudi wakae mezani na kambi ya upinzani na wahakikishe wanapambana pamoja katika kutetea haki za watanzania bila ubaguzi wowote.

Kwa upande wa serikali kuhamia Dodoma mheshimiwa Mdee amesema serikali ihakikishe kwanza inatenga fedha za kutosha za kuhamia Dodoma bila kuathiri bajeti nyingine za serikali ambazo zimetengwa kwaajili ya maendeleo ya nchi.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *