Daktari wa kitengo cha Upasuaji cha Hospitali ya Taifa Muimbili, Dk. Amin Abdulrahmana ambaye ni shahidi katika kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu ‘Scorpion’ leo ametoa ushahidi wake mahakamani.

Dkt. huyo ameiambia mahakama kuwa Saidi Mrisho alitobolewa utumbo mwembamba kwenye tukio hilo.

Dk. Abdulrahmani amesema Septemba 7, mwaka jana saa 12 alfajiri akiwa chumba cha upasuaji alipigiwa simu na kitengo cha dharura cha hospitalini hapo kumtaka kwenda kumhudumia mgonjwa wa dharura.

Amesema kuwa “Baada ya kumfanyia uchunguzi niligundua anahitaji kufanyiwa upasuaji kutokana na jeraha kubwa lililokuwa kushoto mwa tumbo lake lililokuwa na urefu wa sentimita 30 kutoka katika ngozi ya ndani ya tumbo lililotoboa utumbo mwembamba na mengine madogo ambayo yalishonwa na kitengo cha dharura,”.

Pia amesema amefungua tumbo na kuliziba tundu hilo kasha kufunga tumbo na kumpeleka wodi namba 13 na kumpa rufaa kwa wataalamu wa macho kuendelea na uchunguzi wa majeraha ya machoni, Kesi hiyo itatajwa tena Machi 8, mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *