Dada yake mdogo wa aliyekuwa kiongozi wa Cuba, Fidel Castro amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Agustina Castro Ruz hakushiriki katika siasa chini ya ndugu zake wawili, Fidel na Raul ambaye alimrithi Fidel kama rais wa taifa hilo.

Aliolewa na mpigaji kinanda Silvio Rodriguez, aliyelalamika kuhusu uhusiano mgumu na familia ya mkewe.

Rodriguez alihamia nchini Marekani miaka ya 1990 kutokana na kutokuwa na maelewano mazuru na familia ya Fidel Castro.

Dadake mkubwa wa Fidel, Angela Castro alifariki dunia mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 88.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *