Dada wa Raila Odinga, Ruth Odinga anatarajiwa  kushtakiwa kwa kuchochea ghasia baada ya kushambuliwa kwa wafanyakazi wa tume ya uchaguzi IEBC wiki iliyopita.

Ruth Odinga alikuwa ni naibu gavana wa kaunti ya Kisumu nchini Kenya ambaye ameongoza maandamano katika kaunti hiyo.

Mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya Keriakor Tobiko aliamrisha Ruth Odinga akamatwe.

Odinga alikuwa anawania urais pamoja na Rais Uhuru Kenyatta kwenye marudio ya uchaguzi wa urais siku la Alhamisi, lakini aljiondoa mapema mwezi huu, akisema kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa huru na haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *