Serikali ya Marekani imetangaza kuwapeleka wafungwa 15 waliokuwa kwenye gereza la Guantanamo Bay kwenye nchi za Falme za Kiarabu kwenye kipindi cha uongozi wa rais Barack Obama.

Kuachiwa kwa wafungwa hao 15 ambapo wafungwa kutoka Yemeni walikuwa 12 na wafungwa kutoka nchini Afghanistan walikuwa 3 kumelifanya gereza hilo kubaki na wafungwa 61.

Wafungwa walioachiwa walikuwa kifungoni (baadhi yao) kwa zaidi ya miaka 14 huku wakiwa wameshikiliwa bila kufunguliwa mashtaka.

Rais Barack Obama amedhamiria kulifunga gereza hilo lililopo nchini Cuba kabla ya kung’atuka madarakani mwezi Novemba.

Marekani imekuwa ikiwapeleka wafungwa kutoka kwenye gereza hilo kwenye nchi mbalimbali na hivi karibuni mahakama kuu ya Ghana iliiamuru serikali ya nchi hiyo kuweka wazi makubaliano kati yake na Marekani yaliyopelekea wafungwa wawili wa Guantanamo kupelekwa nchini Ghana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *