Klabu ya Crystal Palace imemfukuza kocha wake Frank De boer kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo kwenye ligi kuu chini Uingereza.

De boer ameongoza klabu hiyo kwa siku 77 pekee toka achaguliwa akichukua nafasi ya Sam Allardyce.

Taarifa zilizopo zinasema kuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson atachukua nafasi yake.

Crystal Palace wapo katika nafasi ya 19 katika ligi ya Uingereza kwa kupoteza kwa Burnley 1-0 siku ya Jumapili.

Klabu hiyo imeshindwa kufunga bao lolote latika mechi zao nne za ligi chini ya meneja De boer.

Meneja huyo wa zamani wa Ajax , De Boer , 47 alichukua kazi hiyo ya umeneja mwanzoni mwa msimu huu, baada ya Sam Allardyce aliyeiaga timu hiyo baada ya kuwaepesha katika hatua ya kushushwa daraja msimu uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *