Coutry Boy aitaja ngoma yake anayoikubali zaidi toka aanze kuimba

0
383

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Country Boy amesema kuwa nyimbo yake ya ‘Hakuna matata’ ambayo ameshirikiana na Bill Nas kuwa ndiyo ‘kolabo’ anayoikubali na kuilewa zaidi tangu ameanza kufanya muziki.

Country Boy wimbo huo ni moja ya ngoma anayoikubali zaidi tangu ameanza kufanya kazi na kushirikiana na wasanii wengine na kusema anaupenda wimbo huo kwa kuwa una ujumbe ndani kuwa hata watu wakibana vipi mdogo mdogo watasonga na kufikia malengo.

Mbali na hilo Country boy amedai kwa sasa anajipanga kuachia video ya wimbo huo ambayo huenda ikatoka mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi wa pili.

 

LEAVE A REPLY