Kocha wa Liverpool, Jorgen Klopp amesema kuwa kiungo wake Philippe Coutinho hatokuwepo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Manchester City kutokana na kusumbuliwa na jeraha la kifundo cha mguu.

Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Brazil amekosa mechi sita hadi sasa baada ya kuumia kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Sunderland.

joel-matip-liverpool-wigan-friendly_3746622

Klopp amesema kuwa kiungo huyo uhenda akarejea kwenye mechi dhidi ya sunderland mzunguko wa pili wa ligi hiyo ambayo itachezwa Januari 2 mwakani katika uwanja wa Stadium of Light.

Pia kocha huyo amethibitisha beki wa klabu hiyo Joel Matip atakosa mechi dhidi ya Manchester City kutokana na majeha ya kifundo cha mguu kinachomsumbua kwasasa baada ya kuumia kwenye mechi ya ligi kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *