Mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho amesaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomuweka Anfield mpaka msimu mwaka 2022 ambapo atakuwa analipwa paundi 150,000 kwa wiki.

Kutokana na mktaba mpya aliosaini mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji anayepokea mshahara mkubwa kwa majogoo hao wa Liverpool.

Mshambuliaji huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 aljiunga na Liverpool akitokea Inter Milan ya Italia kwa ada ya uhamisho iliyogharimu paundi milioni 8 mwezi Januari mwaka 2013.

Coutinho amecheza mechi 163 na ameshinda magoli 34 toka ajiunge na Liverpool baada ya kusajiliwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers.

Baada ya kusaini mkataba huo Coutinho amesema kuwa anajisikia faraja kusaini mkataba mpya na kuendelea kubakia Liverpool kwasababu timu hiyo ni kubwa na anafurahia maisha ya Anfield.

Kwa upande wake kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp amesema kuwa anaamini baada ya mshambuliaji huyo kusaini mkataba mpya kumevunja fununu kuwa Coutinho uhenda angeihama timu hiyo mwisho wa msimu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *