Mkali wa hip hop, Country Boy kutoka kundi la Mtu Che amesema kuwa amejikuta katika wakati mgumu baada ya kubwagiwa mtoto na mzazi mwenzake kutokana na kutokuwa na maelewano kati ya wawili hao.

Country Boy amesema kuwa amejifunza kuwa kuna umuhimu kwa mapenzi ya baba kwa mtoto, imezoeleka kwa wazazi wa kiume hutoa pesa tu ya malezi pasipo kuhangaika kwa malezi lakini kwake ameona kuna umuhimu wa mapenzi ya baba kwa mtoto.

Pia amesema amejifunza mapenzi ya mama pia amegundua umuhimu wa mama uko wapi, pamoja na kugundua love ya mtoto na umuhimu wa baba.

Pia Country Boy alizungumza kuwa haoni tatizo kubwa sana kwake pale mtoto wake anapokosa malezi ya pande zote mbili (Malezi ya Mama) na kuamini kuwa siku moja mtoto wake atakuja kuwa mtu mkubwa sana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *