Game ya Hip Hop hapa Bongo imekuwa na historia ndefu sana huku wakongwe kama Mr II na Profesa Jay wakiendelea kushikilia heshima zao kwa waliyoufanyia muziki huo.

Wakati hayo yakiendelea wasanii wengine pia wameendela kuandika historia zao ambazo kwa sasa tunaendelea kuziandika kwa namna mbalimbali.

Ni wazi kuwa mastaa kama Fid Q, Joh Makini, Nikki wa Pili, Nikki Mbishi n.k wanathibitisha kuwa game ya HIP HOP bado mbichi na inalipa ndani ya Bongo.

Lakini wakati wengine wakitaraji kuwa mastaa hao watakuwa kioo kwa mastaa wanaochipukia, rapper Country Boy ameweka wazi kuwa kwa hapa Tanzania rapa anayempa wakati mgumu kidogo ni Bill Nas PEKEEE.

Hata kama ngoma ya MUZIKI au PERFECT COMBO zilikuwa kali, hata kama unaamini Roma Mkatoliki ni NOMA au FID Q ndiye LEGENDARY mpya, lakin kwa Country Boy hao wote si lolote si chochote.

Na katika kulithibitisha hilo, Country Boy amewataja mastaa anaowapa nafasi ya juu kuliko uwezo wake kuwa ni mastaa wa Afrika Kusini ambao ni Emtee anauza, Nasty C, KO, na Cassper Nyovest.

Country Boy anatukana Mamba kabla hajavuka mto? Au anatukana Mkunga wakati uzazi ungalipo?

Ni suala la muda tu……apewe nafasi apate kupimwa kwa vigezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *