Miamba ya soka nchini Hispania Barcelona na Atletico Madrid wanakutana tena leo kwenye mechi ya maruadiano yay a nusu fainali ya kombe la Copa del Rey.

Pambano hilo litachezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Barcelona, Nou Camp lakini hata hivyo msahmbuliaji wa kibrazi wa timu hiyo Neymar atapaswa kulitazama kutoka jukwaani kutokana na kusimamishwa

Timu ya Barca ina faida ya kupata ushindi wa bao 2-1 kwenye uwanja wa Vicente Calderon, ambapo Lionel Messi aliing’arisha Barca.

Atletico Madrid pia watamkosa kiungo wao Gabi ambaye amesimamishwa pia.

Kocha wa Barcelona, Luis Enrique amedai: ‘Wanapaswa kushinda na kufunga angalau kuanzia goli mbili, hivyo tutaiona Atletico ya kushambulia. Wachezaji wangu ni wataalamu wa mechi kubwa’.

Nusu fainali nyingine ni kati ya Alaves na Celta Vigo watakaoshuka dimbani Jumatano hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *