Mwanamuziki wa Rap nchini Marekani, Coolio ameshtakiwa kwa kumiliki bunduki haramu ambapo ni kinyume na sheria ya nchi ya hiyo.

Waendesha mashtaka nchini Marekani wanasema kuwa bunduki hiyo aina ya handgun ilipatikana katika mzigo wake wakati wa ukaguzi katika uwanja wa ndege wa LAX mwezi uliopita.

Coolio mwenye umri wa miaka 53 huenda akahukumiwa kifungo cha hadi miaka 3 katika jela ya jimbo la Carlifornia iwapo atapatikana na hatia.

Coolio ni maarufu kwa wimbo wake Gansta Paradise ambao ulitolewa mwaka 1995.

Waendesha mashtaka wanasema ilikuwa kinyume cha sheria kwa msanii huyo kubeba bunduki baada ya kupatikana na hatia mwaka 2001 kwa kubeba bunduki ndani ya gari na mwaka 2009 kwa kumiliki dawa ya kulevya aina ya Cocaine.

Nyota huyo alitarajiwa kuwasili katika mahakama ya Los Angeles siku ya Alhamisi lakini kusikizwa kwa kesi yake kukaahirishwa hadi Oktoba 26.

Mawakili wa Coolio walimwambia Jaji kwamba msanii huyo alikuwa anawatumbuiza mashabiki wke nje ya jimbo la California na hivyobasi hawezi kuwa katika mahakama hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *