Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema hakuwa anakusudia kumkejeli yeyote baada yake kuonekana akitaka kumkeresha zaidi Jose Mourinho baada ya Chelsea kulaza Manchester United 4-0 jana.

Conte aliwahimiza mashabiki wa Blues kupiga kelele zaidi kuunga timu yake mkono dakika za mwisho za mechi.

Taarifa zinasema kwamba Mourinho alimwambia mkufunzi huyo kutoka Italia kwamba vitendo vyake viliiaibisha United.

Lakini Conte amesema: “Nimekuwa mchezaji pia na najua ninafaa kufanya nini.

Huwa daima namuonesha heshima yeyote, ikiwemo Manchester United.

Mabao ya Pedro, Gary Cahill, Eden Hazard na N’Golo Kante yalivuruga safari ya kwanza ya Mourinho Chelsea tangu afute Desemba mwaka jana kutokana na matokeo mabaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *