Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amesema winga wa Colombia, Juan Cuadrado ni miongoni mwa wachezaji ambao ana mipango nae katika kikosi chake kwa ajiri ya msimu ujao wa ligi kuu nchini Uingereza.

Cuadrado ambaye ni mchezaji wa zamani wa Fiorentina kabla ya kujiunga na Chelsea Februari mwaka jana kwa ada ya uamisho paundi milioni 23.3 lakini alishindwa kushinda hata goli moja katika mechi 13 alizocheza.

Cuadrado alikuwa kwa mkopo kwenye timu ya Juventus msimu uliopita na kushinda magoli 4 katika mechi 28 alizocheza na kuisadia timu hiyo kushinda vikombe viwili.

Conte amesema alikuwa anamuhitaji mchezaji huyo toka alivyokuwa kocha wa Juventus kwa hiyo kwasasa yupo katika timu anayoifundisha na hana budi kumtumia mchezaji huyo raia wa Colombia.

Cuadrado: Akimtoka beki wa Manchester City, Aleksandar Kolarov
Cuadrado: Akimtoka beki wa Manchester City, Aleksandar Kolarov

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *