Mpiganaji wa mchezo wa MMA ‘Mixed Martial Artist’, Conor McGregor amemtusi bondia Floyd Mayweather Jr baada ya staa huyu kushindwa kuonana naye mjini Las Vegas kuongelea pambano lao.

Floyd alimwambia Conor kama anataka pambano kweli basi awasiliane na watu wake sio yeye binafsi.

Conor McGregor ambaye amekuwa akitaka pambano la ngumi na Floyd Mayweather Jr amesema walipanga kukutana mjini Las Vegas kuzungumza ila Floyd hakuonekana.

Conor McGregor ametumia maneno haya kumuelezea mpinzani wake “Floyd’s a b***h and he’s petrified“

Pambano hili limekuwa likishabikiwa na wapenzi wa ngumi za kulipwa na MMA ila mpaka sasa hakuna aliyeweka pesa za kutosha kumshawishi Floyd Mayweather Jr kuingia uwanjani na Conor McGregor.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *