Clouds Media imekanusha tetesi zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa itamleta mwanamuziki wa Marekani, Jay Z kwenye kilele cha Tamasha la Fiesta litakalofanyika katika viwanja vya Leaders  Novemba 5 mwaka huu.

Picha ya mwanamuziki huyo ilisambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha msanii amesajiliwa kawa ajili ya tamasha la Fiesta kitu ambacho Clouds wamekanusha kwamba si kweli na hakuna kitu kama hiko.

Kupitia ukurasa wa instagram Clouds FM umetoa taarifa hii: Kumetokea uzushi kwamba tumemsajili msanii Jay Z kwa ajili ya kilele cha #Fiesta2016 hapo #November05. Tunapenda kukanusha habari hiyo; picha iliyotengenezwa kueneza habari hiyo ni batili.

Wasanii wakimataifa ambao tayari uwepo wao umetangazwa ni Yemi Alade wa Nigeria, Jose Chameleone wa Uganda pamoja na Tekno wa Nigeria.

Tamasha la Fiesta linatarajiwa kufikia tamati Novemba 5 mwaka huu katika viwanja vya Leaders baada ya kumalizika katika mikoa tofauti hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *