Kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri amesema kuwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ni mtu safi na matatizo yaliyokuwepo kati yao kwasasa yameisha na imebaki kama ‘historia’.

Kocha huyo amesema hayo kufuatia tetesi kwamba wawili hao uwenda wakawa na ugomvi lakini kocha huyo amesema taarifa hizo siyo za kweli kwasababu tayari wameshamaliza tofauti zao.

Mgogoro kati ya wawili hao ulianza baada ya Mourinho kuchukua nafasi ya kocha huyo katika klabu ya Chelsea mwaka 2004 na kuanza kumwita Ranieri kama bingwa wa ‘kufeli’ kutoakana na timu hiyo kushindwa kuchuka ubingwa.

Pia vita ya wawili hao iliendelea tena katika ligi ya Italia maarufu kama Seria A wakati Mourinho akiwa kocha wa Inter Milan huku Ranieri akiifundisha Juventus.

Claudio Ranieri amesema mambo yale yameshapita na yamekuwa kama historia kutokana ayana mana kwa kipindi hiki zaidi ya kuangalia mambo mengine.

Wawili hao watakutana kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza ambapo Manchester United itaikaribisha Leicster City katika uwanja wa Old Trafford siku ya jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *