Manchester City imeendeleza wimbi la ushindi kwenye ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuifunga FC Bournemouth jumla ya goli 4-0 katika mechi iliyofanyika katika uwanja wa Etihad jijini Manchester.

Kufuatia ushindi huo City imefikisha jumla ya alama 15 baada ya kucheza mechi tano ya kushinda zote na kufanikiwa kuongoza ligi hiyo yenye ushindani mkubwa kwasasa nchini humo.

Magoli ya Mamchester City leo yamefungwa na  De Bruyne katika dakika ya 15, goli la pili limefungwa na Iheanacho mnamo dakika 25 ya mchezo huo, huku goli la tatu likifungwa na Sterling dakika ya 48 na goli la mwisho limefungwa na Gundogan katika dakika ya 66.

Matokeo mengine ya michezo ya ligi hiyo yalikuwa kama ifuatavyo Hull City walikubali kipigo cha 4-1 kutoka kwa Arsenal, Leicester City wakaifunga Burnley goli 3-0, West Brom wakaitandika West Ham United 4-2.

Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho kwa michezo minne ambapo Mancheser United watacheza dhidi ya Watford, Crystal Palace dhidi ya Stoke City, Southampton ikiikaribisha Swansea City katika uwanja wa St Marry na Tottenham itacheza dhidi ya Sunderland katika uwanja wa White Hart Lane.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *