Video ya wimbo ‘Chura’ ya mwanamuziki, Snura Mushi ambayo ilifungiwa kutokana na kukosa maadili katika jamii sasa imeruhusiwa kutoka baada ya kufanyiwa marekebisho.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kupitia barua kutoka wizara yake ambayo imemruhusu  Snura kuachia video  mpya ya wimbo huo baada ya msanii huyo kufanya marekebisho na kukubaliwa na wizara.

Katika barua ya wizara imemtaka Snura kuomba radhi mbele ya waandishi wa habari ili video hiyo ianze kuchezwa.

Kwa upande wake Snura amesema anamshukuru waziri Nape Nnauye kwa kumkubalia ombi lake la kuiruhusu kazi hiyo kutoka.

Pia katika barua hiyo ya Waziri Nape amempa onyo kali msanii huyo kutokurudia kufanya tena video zisiyokuwa na maadili ya kitanzania.

Mapema mwaka huu video ya wimbo huo ulitangazwa kufungiwa na serikali baada ya video hiyo kukosa maadili ya kitanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *