Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya kimefungwa kwa muda usiojulikana kwasababu za kiusalama.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya siku kadha za wasiwasi uliotokana na makabiliano kati ya wanafunzi na polisi wa kukabiliana na fujo ndani ya chuo hicho.

Polisi waliingia chuoni walipokuwa wakikabiliana na wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulalamikia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa chuo hicho Paul Ongili, maarufu kama Babu Owino.

Babu Owino, ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Embakasi Mashariki jijini Nairobi, alikamatwa baada ya kudaiwa kumtukana Rais Uhuru Kenyatta.

Baadaye alikamatwa tena na kufunguliwa mashtaka mengine ya kumshambulia mpiga kura wakati wa uchaguzi mwezi Agosti.

Wanafunzi takriban 26 walijeruhiwa ambapo video ambazo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni zimeonyesha maafisa wa polisi wakiwafurusha wanafunzi kutoka kwa vyumba vya malazi na hata kwenye madarasa.

Mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema kufikia sasa ni vigumu kubaini iwapo video hizo ni za kweli na iwapo wanaoonekana wakipigwa na maafisa wa polisi ni wanafunzi.

Mamlaka inayosimamia utendakazi wa polisi na kutetea haki za raia (IPOA) imetoa wito kwa wanafunzi 26 ambao walijeruhiwa kuandikisha taarifa.

Njeru alisema baada ya uchunguzi, wamebaini nyingi za video na picha ambazo zinaenezwa mtandaoni zikidaiwa kuwaonesha polisi wakiwashambulia wanafunzi ni za uzushi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *