Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Chuchu Hans amefunguka kwa kusema kuwa yeye na mpenzi wake Ray Kigosi hakuna anayewaza ndoa.

Chuchu Hans amesema hayo baada ya watu kuhoji lini itafanyika ndoa ya wawili hao ambao wameingia kwenye mahusiano kwa muda mrefu.

Pia amesema kuwa yeye na Ray hawajakaa na kulizungumzia suala la ndoa lakini anaamini kuwa siku ikifika mambo yatakuwa sawa na ndoa itafanyika.

Chuchu Hans akiwa na mpenzi wake Ray Kigosi
Chuchu Hans akiwa na mpenzi wake Ray Kigosi.

Amesema kuwa “Hakuna hata mmoja kati yetu anayeiwazia ndoa. Sasa hivi kila mtu jicho lake lipo kwa mtoto na naamini siku ikifika Ray mwenyewe atazungumza kwa kuwa jambo hili halitaki kulazimishwa hata siku moja,”.

Wawili hao wamefanikiwa kupata mtoto wao mmoja wa kiume anayeitwa Jaden aliyezaliwa mwanzoni mwa mwaka huu.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *