Msanii maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Christina Shusho ameomba radhi kwa wakenya baada ya kuposti maneno yaliyowakera wapinzani wa Rais Uhuru Kenyatta.

Muimbaji huyo kupitia ukurasa wake wa Facebook siku ya Jumamosi aliandika maneno yalisomeka ‘Mungu mpe mtumishi wako Uhuru Kenyatta busara na jibu maombi yake wakati akikuomba.

Pia ameendelea kuandika ‘Mpe upeo wa kuongoza nchi ya Kenya na mjibu maombi yake pale anapokuomba.

Baada ya kuandika hivyo, wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga wamekosoa machapisho hayo ya mwanamuziki huyo kwa kuhoji kwanini maombi yake yamebase upande mmoja.

Muimbaji huyo amesema kuwa ilikuwa siyo nia yake ya kuwahudhi wafuasi wa Raila Odinga kwani yeye alifanya hivyo kama maombi kwa Rais huyo.

Odinga amejitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa marudiano utakaofanyika kesho nchini Kenya baada ya matokeo ya awali yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta kutenguliwa na mahakama kuu nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *