Staa wa muziki wa dansi nchini, Christian Bella amesema amepata shida sana wakati wa kurekodi wimbo wa msanii wa Hip Hop, Fid Q unaoitwa ‘Roho’ kutokana na ugumu wa mashairi kwenye wimbo huo.

Christian Bella amesema ilimbidi aombe atafsiriwe maana ya maneno ya kwenye mashairi ya wimbo wa ‘roho’ wa Fid Q ili aweze kuandika maneno ya kuimba kwenye kiitikio chake hata hivyo aligonga mwamba.

Muimbaji amesema alipoambiwa aende akapige chorus kwenye nyimbo ya Fid Q ambayo alikuwa anarekodi kwa P Funk Majani akapiga mahesabu kwakujua kwamba Fid Q yeye ni mtu wa hip hop ngumu jeje hataweza kufanya nae ngoma.

Bella akaendelea kusema kwamba kwa kuwa alikuwa anamuheshimu sanaFid Q na pia anamkubali kwa hiyo ikabidi aende tu kufanya nae nyimbo lakini alipata tatbu sana mpaka akaamua atafsiriwe baadhi ya maneno kwenye nyimbo hiyo.

Vile vile Christian Bella amesema kuwa msanii huyo tungo zake ni ngumu kuzielewa mara moja na kwamba ndiyo kitu kilichompa ugumu kwenye kurekodi collabo yao ambayo inafanya vizuri kwenye media tofauti za hapa bongo kwa hiv sasa hivi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *