Mwanamuziki nyota wa Marekani, Chris Brown amevunja simu ya shabiki mmoja mara baada ya kuwasili nchini Kenya kwa tamasha la muziki mjini Mombasa.

Shabiki huyo mwanamke anamtuhumu Chris Brown ameivunja simu yake alipojaribu kupiga picha ‘selfie’ alipowasili katika uwanja wa ndege Mombasa.

Mwanamke huyo amesema Chris Brown alimpokonya simu kutoka nyuma alipojitayarisha kuipiga picha hiyo na kuirusha chini.

Shabiki huyo amesema kuwa simu yake ni aina ya iPhone 6 iliyomgharimu takriban dola 900, haikuvunjika lakini kizuia kioo na kifunikio cha simu viliharibiwa.

Brenda Chepkoech: Mwanamke aliyevunjiwa simu na Chris Brown akionesha jinsi mwanamuziki huyo alivyoiharibu.
Brenda Chepkoech: Mwanamke aliyevunjiwa simu na Chris Brown akionesha jinsi mwanamuziki huyo alivyoiharibu.

Pia shabiki huyo amesema amenunua tiketi kuhudhuria tamasha hilo lakini ameghadhabishwa na tukio hilo na ameamua kutohudhuria tamasha hilo.

Tuhuma zake zimesababisha gumzo katika mtandao wa Twitter kupitia #DeportChrisBrown ambapo Wakenya wanajadili iwapo muimbaji huyo nyota arudishwe Marekani.

Kanda ya video iliyowekwa na @KinyanBoy katika twitter inaonekana kumuonyesha Chris Brown akipuuza ombi la mwanamke huyo kupiga selfie na anampita bila kumgusa.

Lakini mwanamke huyo aliyejitambulisha kama Brenda Chepkoech, amesema kuwa tukio hilo limetokea baada ya kanda hiyo kuwekwa kwenye mtandao na ni muda mfupi kabla ya CB kuingia garini na kuondoka.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *