Mwanamuziki nyota wa Marekani, Chris Brown ameamua kumuomba msamaha mpenzi wake wa zamani Karruche Tran kupitia akaunti yake ya Instagram.

Mapenzi ya wawili hao yalivunjika tangu mwezi Machi 2015, baada ya msanii huyo kuletewa mtoto wa miezi tisa ambaye alimpa jina la Royalty, mtoto huyo alimpata na mrembo mwingine ambaye alijulikana kwa jina la Nia Guzmann.

Baada ya Chris kuachana na mrembo huyo amedaiwa kutoka na mwanamitindo Krista Santiago lakini cha kushangaza msanii huyo amemwomba radhi Karrueche.

Kupitia akaunti yake Instagram Chris Brown ameandika “Nilikuzoea, tulikuwa wote sehemu mbalimbali, naomba tuyasahau hayo,”.

Maneno ya msanii huyo yanadaiwa kumweka katika wakati mgumu kwa mpenzi wake wa sasa, Krista.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *