Staa wa muziki nchini Marekani, Chris Brown amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia mtu kwa silaha hatari.

Polisi walifika katika makazi ya Chris Brown baada ya mwanamke kuwapigia simu kwa kuwaomba msaada saa tisa usiku wa kuamkia leo.

Mwanamitindo nchini Marekani, Baylee Curran ameambia gazeti la LA Times kwamba mwanamuziki huyo alimwelekezea bunduki.

Hata hivyo Polisi hao walizuiwa kuingia na ilibidi wasubiri hadi kupata idhini ya jaji kabla kufanya msako wa kutafuta bunduki katika makaazi hayo.

Mwanamke huyo aliyewaita polisi baadaye aliambia vyombo vya habari kwamba walitofautiana na Brown kuhusu majohari.

Baylee Curran: Mwanamke aliyetishiwa bunduki na Chris Brown.
Baylee Curran: Mwanamke aliyetishiwa bunduki na Chris Brown.

Mwanamke huyo amesema alikuwa ameingia kwa Chris Brown akiwa na rafiki yake na mshirika wa kibiashara na alikuwa akiangalia mkufu wa thamani uliokuwa umevaliwa na mwanamume mmoja pale mwanamuziki huyo alipomkaripia na kumtaka aondoke mara moja akiwa amemwelekezea bunduki.

Chris Brown ameandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kujitetea na kuwalaumu polisi kwa kumhangaisha.

Wakili wake alifika kwenye makaazi hayo na kumsihi aandamane na maafisa wa polisi. Mwanamziki huyo anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya uvamizi.

Chris Brown amewahi kujipata matatani awali hususan alipomshambulia aliyekuwa mpenzi wake na mwanamziki Rihanna hapo Februari 2009.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *