Mwanamuziki nyota wa Marekani, Chris Brown amesema kuwa kuna watu wanauza habari zake za kila siku kwenye mtandao wa TMZ.

Brown amesema anashangaa kuona baadhi ya mambo yake anayoyafanya kila siku lazima wayapate TMZ, hivyo anaamini kuna watu ambao wanapiga pesa kupitia habari zake.

TMZ ni tovuti ambayo inaelezea habari mbalimbali za watu maarufu, mtandao huo ulianzishwa Novemba 8, mwaka 2005 na kazi yao kubwa ni kununua stori na kuzisambaza.

Mwanamuziki amesema kuwa “Kuna watu wanaofuatilia maisha yangu kuanzia naamka nadi nalala, baadhi ya mambo ambayo ninayafanya kila siku nayaona TMZ.

Chris Brown amesema kuwa ‘nanaamini kuna watu wanauza habari zangu, maisha yao yanakwenda sawa kwa ajili yangu, ipo siku nitawanasa,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *