Staa wa muziki nchini Marekani, Chris Brown ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa kwa kosa la kumtishia bunduki mwanamke aliyejulikana kwa jina la Baylee Curran.

Staa huyo ametoka kwa dhamana ya $250,000 baada ya kukamatwa kwa madai ya kumtishia mtu na silaha.

Baylee Curran alimshutumu Brown kwa kumtishia na bunduki yake huko Tarzana, Calif.

Mrembo huyo aliyekuwa akijirusha na Brown kabla ya hapo, anadai kuwa ugomvi ulizuka baada ya kuonesha kutamani midani zake za madini.

Muimbaji huyo alidaiwa kumfukuza msichana huyo na kumtishia na bunduki.

Maofisa wa polisi waliwasili kwenye eneo la tukio saa tisa alfajiri Jumanne hii baada ya simu ya 911 kupigwa na mwanamke aliyehitaji msaada.

Curran alipeleka mashtaka polisi na kukatolewa hati ya kufanywa msako.

Wakati wa uchunguzi, Brown anadaiwa kutupa begi lake dogo nje ya dirisa ambamo kulikuwa na bunduki mbili na madawa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *