Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini, Ali Choki amewashukuru wanamuziki wenzake pamoja na amashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la kutimiza miaka 30 tangu aanze kuimba muziki.
Ali Choki amewashukuru wasanii ambao alishirikiana nao katika kipindi chote hicho cha muziki wake.
Pia Choki amesema anashukuru sapoti aliyoipata kutoka kwa wanamuziki wenzake kama Zahir Zoro, Komando Hamza Kalala na wengine lakini pia aliamua kupiga nyimbo za Extra Bongo ili kuonesha maana ya halisi ya miaka 30 ya Choki.
Vile vile Choki amesema huenda akapumzika baada ya miaka 20 ijayo mbele japo hawezi kusema rasmi kwamba ataacha muziki kwa kuwa siyo rahisi kustaafu muziki kwani muziki ni kipaji chake labda akifikisha miaka 50 ya muziki.
Mwanamuziki huyo ambaye kwasasa yupo katika Bendi ya African Stars ( Twanga Pepeta) ameanza kuimba toka mwaka 1986 baada ya kupita bendi kibao hapa nchini kama vile Extra Bongo, Twanga Pepeta, TOT Plus pamoja na Mchinga Sound.