Mwanamuziki wa dansi nchini, Khalid Chokoraa amewataka wanamuziki wa singeli nchini kuacha kuuchukulia muziki huo uhuni badala yake wachukulie kama kazi.

Chokoraa ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta kwasasa ameamua kuingia kwenye muziki wa singeli.

Chokoraa amesema “Kikubwa zaidi nawasihi wasanii wa kisingeli kuangalia maneno wanayoyatumia na kupunguza maneno ya mtaani ili tuelimishe kupitia kisingeli”.

Chokoraa amesema wasanii wa sengeli ambao anatamani kuimba nao ni Sholo Mwamba, Man fongo na Dullah Makabila.

Pia mwanamuziki huyo amesema kwamba anatarajia kuachia video yake mpya hivi karibuni na kuwataka mashabiki zake kuisubiri kwa hamu kwa kuwa wimbo huo unaelimisha, unaburudisha na una ujumbe mzuri kwa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *