China imeonya kwamba huenda uhusiano wake wa siku zijazo na Uingereza ukatatizika ikiwa mradi wa mabilioni ya dola wa ujenzi wa mtambo wa nyuklia hautaendelea.

China inatarajia kudhamini theluthi moja ya ujenzi uliopangwa wa kiwanda cha nyuklia wa Hinkley Point kusini mwa Uingereza.

Lakini mwezi uliopita serikali ya Uingereza ilitangaza kuutathmini upya mradi huo kufuatia hofu iliyopo ya hali ya usalama kuhusu kuhusishwa kwa Uchina.

Balozi wa Uchina mjini London Liu Xiaoming ameitaka serikali ya Uingereza kufanya uamuzi wa mwisho haraka huku akisema kuwa uhusiano baina ya Uingereza na China uko njia panda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *