Majibu hayo ya hasira yanajiri baada ya waziri mteule wa mambo ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kusema kuwa Marekani inapaswa kuizuia Beijing kuingia katika visiwa vipya katika bahari ya kusini mwa China.
Beijing imekuwa ikitengeneza visiwa katika miamba ya maji yanayogombaniwa na mataifa mengine.
Picha zilizochapishwa mwaka uliopita zinaonyesha ulinzi mkali katika baadhi ya visiwa hivyo.
Tillerson aliifananisha visiwa hivyo vya China na hatua ya Urusi kuchukua eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine.