Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chin Bees ameweka hadharani msimamo wake wa kutothubutu  kushirikiana na  kundi la ‘Navy Kenzo’ kwa madai kuwa walishindwa kumpatia heshima aliyoihitaji kipindi alipokuwa katika mikono yao.

Chin Bees amefunguka hayo baada ya kuwepo maswali mengi mtaani kama ataweza kufanya kazi na kundi hilo iwapo  itatokea akatakiwa tena  kurudi ndani ya mikono ya wasanii hao, na kusema ni bora apambane peke yake kuliko kufanya kazi ya kuwanufaisha watu.

Pamoja na hayo Chin Bees alisema “Hata mkataba wangu ukiisha Wanene kuliko kurudi kwa Navy Kenzo nitaendelea kupambana peke yangu kuliko kwenda kufanya kazi na watu ambao wao wanfanikiwa kupiti mgongo wako wewe ukiendelea kubaki mtupu mifukoni.

Aidha Chin Bees ameongez kwa kutoa shukrani kwa kundi la Weusi kwa kumuamini na kumpatia nafasi kwenye nyimbo mbili kubwa kitu ambacho kiliweza kumtambulisha vizuri kwenye game na kuweza kujiongezea mashabiki.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Mimi ma-brothers nitawashukuru sana maana nilivyoondoka kwa Navy Kenzo walinishika mkono kwa kunipa sapoti, kwanza waliniamini kwenye wimbo wa ‘Arosto’ ambao kwangu mimi ulinipa nafasi ya kutambulika vizuri na kwenye Sweet Mangi  vile vile, nawaheshimu sana kaka zangu Weusi kwa sapoti yao kwangu.

Chin Bees kwa sasa anatamba na ngoma ya Nyonga nyonga, ukiacha Trap ya Pepeta inayozidi kusumbua masikio ya wapenda burudani.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *