Kila sifa iliyo njema inamstahiki Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani na nje yake ambaye ndiye mkamilifu kwa kila hali.

Sisi binadamu ni viumbe ambao licha ya kupewa uwezo na upendeleo mkubwa sana na Mwenyezi Mungu ikiwemo akili lakini bado ni sehemu ya maumbile yetu kufanya makosa mbalimbali lakini baada ya kukosea huwa tunajifunza ili tusiyarejee makosa yale yale wakati mwingine.

Je, Chidi Benz amejifunza?

Rapa na staa wa Hip Hop kwenye muziki wa Bongo Fleva, Chidi Benz ni msanii ambaye uwezo wake mkubwa wa kurap, kutunga na kuamsha amsha mashabiki uko wazi mbele ya wapenzi wa Bongo Fleva.

Ushahidi wa uwezo mkubwa alionao Chidi unajidhihirisha kwenye ngoma zake kadhaa ikiwemo ‘Dar es Salaam STAND UP’ huku uwezo huo pia ukionekana kwenye ngoma mbalimbali alizoshirikishwa ikiwemo USINIACHE ya Spack.

9e87d543-e679-4b7c-8a25-76c9318ea142

Baada ya kutamba sana kwenye gemu ya Bongo Fleva, Chidi Benz akaanza kukumbwa na kashfa mbalimbali za utovu wa nidhamu hadi kuhukumiwa kwenda jela kabla ya familia yake kumlipia faini na kumnusuru na adhabu hiyo.

Mbali ya kashfa hizo, Chidi Benz akaanza kuvuma kwa utumiaji wa dawa za kulevya, na kama ilivyo ada ya wengi, taarifa hizo hukanushwa na vikali na wahusika wakuu. Baada ya kipindi kirefu cha tetesi hizo hatimaye Chidi Benz akajitokeza hadharani na kukiri kuwa yeye ni muathirika wa dawa za kulevya na akaomba msaada ili aweze kunusurika na janga hilo.

Mungu si Athumani, hatimaye Chidi Benz akapata msaada mkubwa kutoka kwa wadau wa muziki na wanaharakati wa vita dhidi ya dawa za kulevya na kupelekwa kwenye kituo cha msaada kwa waathirika wa dawa za kulevya ambapo baada ya kuishi huko kwa takribani mwezi Mmoja, Chidi akaruhusiwa kutoka akiwa na afya salama.

Lakini katika kipindi ambacho Chidi alipelekwa kwenye kituo hicho, mambo mengi yalizungumzwa na watu mbalimbali waliweka wazi maoni yao juu ya hatua ya Chidi kuingia kwenye janga hilo hadi wale waliojitolea kumsaidia nao waliguswa (kwa namna nzuri na mbaya pia).

Sasa, Chidi ameonekana tena akiwa na afya nzuri, yuko salama, Chidi amerudi kwenye hali yake ya ung’avu na uchangamfu………MUNGU MKUBWA!

Je, Chidi Benz amejifunza? Amejifunza kutokana na mkasa uliomkuta? Amejifunza kutokana na wema aliotendewa?Amejifunza kutokana na maoni hasi na chanya yaliyotolewa kumhusu yeye? Chidi amejifunza kuhusu thamani yake kwenye muziki na jamii? Chidi amejifunza kuhusu athari na madhara ya dawa za kulevya?

Kujifunza ni jambo moja LAKINI kujutia makosa ni jambo tofauti sana, Chidi anapaswa KUJUTIA MAKOSA YAKE kisha ADHAMIRIE KUTOYARUDIA TENA!

Yaliyosemwa yamesemwa na yaliyotokea yametokea TUGANGE YAJAYO Chidi!!

Let’s hope kuwa ‘UMEJUTIA KOSA LAKO NA UMEJIFUNZA KUPITIA STORI YAKO MWENYEWE’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *