Staa wa Hip-Hop nchini, Chidi Benz amesema meneja wa Tip Top Connection na Diamond Platnum, Babutale ni mtu mwenye umuhimu wa aina yake na atamheshimu daima kwasababu meneja huyo ametumia fedha nyingi kwa ajili yake.

Chidi Benz amesema huwezi amini mpaka sasa hivi Babutale anaweza akawa ametumia milioni 45, 50, 60 kwa vitu ambavyo vimefanyika tayari, lakini bado ajasaini mkataba wowote na meneje huyo.

Staa huyo pia anadai kuwa anamchukulia Babutale kama familia yake kwasababu hata sasa hivi anakaa kwa meneja huyo.

Babutale alimsaidia Chidi Benz kuepukana na uraibu wa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kumpeleka rehab na baada ya kutoka hivi karibuni kaingia studio kurekodi nyimbo mpya aliyomshirikisha Raymond inayoitwa “Chuma”.

Chidi Benz: Akiwa na Babutale na Kala Pina.
Chidi Benz: Akiwa na Babutale na Kala Pina.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *