Chid Benz kuja na albam mpya

0
67

Mwanamuziki wa rap Bongo Rashid Makwiro maarufu kama Chid Benz ameachia tracklist ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ijayo aliyoipa jina la ‘Wa2 Wangu’.

Mwanamuziki huyo ameamua kuachia orodha ya nyimbo zake kwenye albam hiyo mpya baada ya kukaa kimya muda mrefu bila kuachia albam.

Chidi ameachia tracklist ya nyimbo 18 ikionekana kuwa wasanii walioshirikishwa ni pamoja na mwanakikundi cha muziki wa rap ‘Wakadinali’ kutokea Kenya, Baddest 47, Only1pabo na Brian Simba kutokea Tanzania.

Chid Benz amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea albam hiyo kwani amewaandalia nyimbo kali ambazo huwezi kuchoka kuzisikiliza ndani ya albam hiyo.

LEAVE A REPLY